ZINAZOVUMA:

Kada wa CCM Arusha afariki Dunia

Kada na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha amefariki Jijini...

Share na:

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ndugu Zelothe Stephen, amefariki dunia leo tarehe 26 Oktoba 2023.

Zelothe amefariki alipokuwa Jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Marehemu aliwahi pia kuwa Afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

Taarifa hii pia imethibitishwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo Jerry Silaa, katika ukurasa wake wa Instagram.

“Kwa masikitiko makubwa, kwa niaba ya familia, naomba kuleta taarifa za kifo cha Mzee Zelothe Steven kilichotokea leo Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu”. Aliandika Mhe. Jerry Silaa.

Na kuongeza kuwa mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Upanga Seaview.

Na mazishi yatafanyika nyumbani kwake Olasiti Arusha kwa tarehe itakayopangwa.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,