ZINAZOVUMA:

Congo: Tshisekedi anaongoza uchaguzi wa Urais

Tshisekedi wa Congo ambwaga Katumbi kwenye uchaguzi, Hadi sasa anaongoza...
Rais Felix Tshisekedi wa DRC (kulia), akiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame (Kushoto) na Rais wa Angola Joao Lourenco (kati).

Share na:

Zaidi ya kura milioni 12 zimehesabiwa baada ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu nchini Congo, na hadi sasa Rais aliye madarakani Tshisekedi anaongoza zaidi ya kura milioni 9.

Anayefuata kwa kura nyingi ni Moise Katumbi mwenye Milioni 2 sawa na 16.5% ya kura zilizohesabiwa, na watatu ni Martin fayulu mwenye kura Laki tano sawa na 4.4% ya kura zilizohesabiwa.

Wagiombea wengine hawajafikisha kiasi cha kura laki moja na 25 ambayo ni sawa na asilimia moja ya kura zilizohesabiwa.

Mbali na kuwa zaidi ya watu milioni 40 wamepiga kura, wachambuzi wengi wa kisiasa nchini humo wanaona Tshisekedi atashinda uchaguzi huu.

Martin Fayulu amesema hawatakubali matokeo ya uchaguzi huu ambao umejaa wizina matokeo ya kupangwa.

Matokeo ya jumla ya uchaguzi huu yanatarajiwa kutolewa tarehe 31 na Tume ya uchaguzi nchini humo.

Na mwezi Januari inangojwa Mahakama ya kikatiba itatoa maamuzi gani juu ya matoke hayo ya tume ya uchaguzi.

Kanisa Katoliki na la kiprotestanti nchini Congo yalikuwa kama waangalizi na wametoa ripoti yao ya matokeo wanayoamini kuna changamoto katika uchaguzi.

Na kuongeza kuwa changamoto hiyo ni mgombea mmoja kuwa na zaidi ya nusu ya kura zote.

Huku wapinzani wakiwa tahadharisha wafuasi wao kuwa macho na wizi unaoweza kufanywa na serikali.

Inahofiwa nchi kuingia katika machafuko yatakapotangazwa matokeo yote.

Katika kuondoa hofu iliyotanda nchini humo serikali imetangaza kupitia msemaji wake Patrick Muyaya kuwa imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama nchini humo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya