ZINAZOVUMA:

Boeing na AirBus zashauriwakuharakisha uzalishaji

Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege la Qatar Airways ameyashauri...

Share na:

Mtendaji mkuu wa shirika la ndege la Qatar Airways Badr Mohammed Al Meer, ameshauri kampuni za kuzalisha ndege za Boeing na Airbus kuongeza uzalishaji wa ndege.

Al meer amewataka makampuni hayo kuwabana wazabuni wake ili wapunguze kuchelewesha vipuri vya uzalishaji wa ndege, ili kuweza kutoa oda za wateja kwa wakati.

Kampuni hizo hizo zimekuwa zimeshindwa dwa kuendana na kasi ya uhitaji wa ndege mpya duniani, tangu wimbi la Corona kupungua na safari za ndege kuongezeka.

Hata hivyo miongoni mwa sababu zinazofanya kampuni hizo kushindwa kupata vipuri na mahitaji mengine kwa wakati ni hali ya usafiri na ugavi duniani pamoja na changamoto za kiusalama zilizoikumba kampuni ya Boeing.

Mtendaji mkuu huyo wa Qatar Airways aliyasema hayo katika mkutano wa Qatar Economic Forum uliofanyika Mei 15 jijini Doha.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya