ZINAZOVUMA:

Mashirika ya Ndege kurudisha safari za Mashariki ya Kati

Mashariki ya Kati imeanza kufunguka baada ya mashirika ya ndege...

Share na:

Mashirika ya ndege ya Mashariki ya Kati yalitangaza kuwa yameanza tena safari zao katika eneo hilo baada ya kuziahirishwa au kubadilishwa kwa baadhi ya safari hizo.

Mvurugano huu wa safari za ndege katika eneo hilo ulikuja baada ya Iran kurusha ndege zisizo na rubani pamoja na makombora kuelekea Israel.

Msemaji wa shirika la ndege la Emirates alisema kuwa Hadi Jumapili mchana, shirika hilo la ndege lilikuwa likirejesha ratiba zake za safari za kwenda na kutoka Iraq, Jordan na Lebanon.

Kutokana na shambulizi za Iran dhidi ya Israel shirika hilo kubwa zaidi Mashariki ya Kati, lilifuta baadhi ya safari zake za ndege baada ya nchi nyingi za eneo hilo kufunga anga kwa muda.

Qatar Airways pia ilirejesha ratiba zake za ndege huko Amman, Baghdad na Beirut, ilichapisha kwenye ujumbe wake kupitia mtandao wa X.

Shirika la Ndege la Etihad lenye makao yake makuu Jijini Abu Dhabi, lilitangaza kuwa litaanzisha upya safari zake za abiria na mizigo kati ya Abu Dhabi na Tel Aviv, Amman na Beirut leo Jumatatu.

Mbali na kufungua huduma, Shirika hilo la Etihad lilitahadharisha kuwa kutokana na kufungwa kwa anga maeneo mengi kwenye ukanda huo wa Mashariki ya Kati, wanaweza kujikuta wanatoa huduma chini ya uwezo wao siku hiyo ya jumatatu.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya