ZINAZOVUMA:

Marubani wa Air Tanzania kuwafundisha wa Nigeria

Marubani wawili kutoka Air Tanzania wanatarajiwa kuwafundisha wenzao wa Ibom...

Share na:

Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) limeingia makubaliano ya kupeleka marubani wake kufundisha na kusimamia ndege mpya za Airbus A220 za Kampuni ya Ndege Ibom nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania, Ladislaus Matindi alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa wametoa marubani waandamizi wawili, ili wa kuwafundisha kwa vitendo marubani na walimu wa marubani wa Ibom Air kwa muda wa miezi sita.

“Marubani wa wetu watakuwa na jukumu la kufundisha na kusimamia mafunzo kwa vitendo hadi watakapo jiridhisha kuwa marubani wanafunzi na walimu wao wamefikia viwango vinavyotakiwa kurusha ndege hizo” alisema.

Aidha, Kampuni ya Ibom Air italipa gharama za mafunzo hayo, kwa mujibu wa mkataba kwa kipindi chote cha makubaliano.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya ATCL kuonesha uzoefu kumiliki ndege za Airbus A220-300 kwa muda mrefu pamoja na kuridhishwa na kiwango cha umahiri wa marubani wa wa shirika hilo.

Mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo kwa marubani wa Ibom Air watakaorusha ndege za Airbus A220, ambazo ATCL ina uzoefu wa miaka mingi wa kumiliki ukilinganisha na Ibom Air ambao ndio wanaanza kutumia ndege za aina hiyo.

ATCL ina zaidi ya marubani 100, inamiliki ndege aina ya Boeing B787-8, B737 MAX 9, B767-300F, Airbus A220-300 pamoja na Dehaviland Q400 na Q300.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya