ZINAZOVUMA:

Ye Htut waziri wa zamani wa habari akamatwa Myanmar

Ye Htut: Waziri wa Habari wa serikali ya kijeshi ya...

Share na:

Ye Htut, waziri wa serikali ya kijeshi iliyokabidhi madaraka kwa bi Aung Suu Kyi mwaka 2015, amekamatwa kwa kosa la uchochezi mtandaoni.

Waziri huyo alishikilia wadhifa wa waziri wa Habari na pia alikuwa Msemaji wa Serikali ya kipindi hicho.

Serikali ya sasa ya Kijeshi imeema kuwa Ye Htut alikamatwa jumamosi jioni kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mitandaoni.

Juma lililopita chaneli ya telegram inayounga mkono serikali ya kijeshi, ilimtaja Ye Htut kama chanzo cha kuvuja kwa anuani ya kiongozi mstaafu wa jeshi katika mitandao ya kijamii.

Waziri huyo aliyezoeleka kwa kuchapisha katika mitandao ya kijamii, na hata serikali yao ya kijeshi haikukandamiza haki za kujieleza katika mitandao ya kijamii.

Na yeye kupewa jina la utani “Facebook Minister” yaani waziri wa Facebook kutokana na kuchapisha kwake mara kwa mara katika mtandao huo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya