ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu aagiza wanaowahujumu wakulima wakamatwe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kuwa watendaji wote wanaobainika kuiba...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza watendaji wote watakaobainika kuiba pembejeo za kilimo wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanaihujumu Serikali.

Pia amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Deogratius Mbowe amuhoji Afisa Kilimo wa Kata ya Kitama, Sharaf Manjavila kwa tuhuma za kuchukua pembejeo za Wakulima.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo mkoani Mtwara wakati akizungumza na Wananchi baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kitama wilayani Tandahimba.

Awali, baadhi ya Wananchi walimuomba Waziri Mkuu aondoke na Afisa Kilimohuyo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake ikiwemo kumtuhumu kuiba pembejeo za wakulima wa korosho.

Wakulima hao walidai kuwa walifanyiwa uhakiki na kupewa namba, ila wanapokwenda kuchukua pembejeo wanaambiwa hawajasajiliwa na majina yao hayajarudi, hivyo hawapewi dawa.

Waziri Mkuu amewahakikishia Wananchi hao kuwa Serikali itahakikisha suala hilo linasimamiwa vizuri, hivyo waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya