ZINAZOVUMA:

Waziri Mhagama: Ondokeni maeneo hatarishi

Waziri Jenista Mhagama awataka wananchi wa Halmashauri ya Mlimba kuondoka...

Share na:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amewataka wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi ili kujikinga na madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Ametoa kauli hiyo wakati alipotembela maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro, ambapo amewaomba wananchi kuendelea kushikamana na serikali ili kuweza kupambana na majanga ya mafuriko katika maeneo yao.

Aidha Mhagama amewaomba wananchi hao kuendelea kumuomba mwenyezi mungu, ili waweze kupita katika kipindi hicho kigumu kwa haraka na kwa usalama zaidi.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali imetengeneza mpango wa kukabiliana na vipindi mbalimbali vya mvua, ilikuweza kuzuia madhara yasijitokeze hususani kuokoa maisha ya Watanzania.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya