ZINAZOVUMA:

Zaidi ya 29 wafariki kwa mafuriko China

Idadi ya watu waliofariki na mafuriko inazidi kuongezeka kaskazini mashariki...

Share na:

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko katika mkoa wa Hebei kaskazini mwa China imeongezeka na kufikia hadi watu 29.

vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki huku wengine wakiwa hawajulikani walipo baada ya kunyesha mvua kubwa katika eneo hilo katika wiki za hivi karibuni.

“Tangu Agosti 10, watu 29 wamefariki kutokana na majanga katika mkoa wa Hebei, ambapo 6 hawajulikani walipo na Kufikia sasa idadi ya watu waliokosekana ni 16,” shirika la utangazaji la serikali CCTV limeripoti, likinukuu mamlaka ya mkoa wa Hebei.

Aidha takriban watu 33, wakiwemo wafanyakazi wawili wa uokoaji, walifariki mjini Beijing kutokana na dhoruba kali na mafuriko mwishoni mwa mwezi uliopita.

Lakini pia zaidi ya watu kumi na wawili walifariki katika jimbo la Jilin, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya mvua kubwa kunyesha wiki iliyopita.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya