Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga aliyeitisha maandamano ya siku tatu akiwataka kuandamana, ili kupinga gharama za juu za maisha yameanza katika maeneo tofauti nchini Kenya.
Tayari makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yameanza kushuhudiwa katika eneo la kibera mjini Nairobi, ambapo maafisa wa polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa watu wawili mpaka sasa, wamepigwa risasi na kupata majeraha wakati maandamano yakiendelea katika Kaunti ya Migori.
Msimamizi wa hospitali huko Migori, Oruba Ochere amethibitisha kuwa wanaume wawili ambao wamejeruhiwa kwa risasi wanapokea matibabu katika hospitali hiyo.
Ochere amesema mmoja wa waathiriwa amepigwa risasi ya paja, huku mwingine akiwa kapigwa risasi ya mguu.