ZINAZOVUMA:

Waisrael waandamana kumpinga Netanyahu

Waisrael waingia mtaani kuipinga serikali ya Netanyahu na kutaka mateka...

Share na:

Makundi ya waisraeli Waandamanaji waliingia mitaani katika jiji la Tel Aviv Alhamisi usiku kupingana na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu na kutaka kuachiliwa kwa makumi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.

Waandamanaji hao walibeba picha kubwa za mateka pamoja na mabango yenye kauli mbiu zilizoandikwa kiingereza na kiebrania.

Mwanzoni mwa mwezi huu, makumi ya maelfu ya Waisraeli waliandamana katikati ya Jerusalem kuipinga serikali tangu nchi hiyo ilipoingia vitani mwezi Oktoba.

Takriban miezi sita ya mzozo imezusha mgawanyiko juu ya uongozi wa Netanyahu, ingawa nchi hiyo inasalia kuendelea na vita.

Waziri mkuu huyo wa Israel anasema uchaguzi haraka utailemaza Israel kwa muda wa miezi sita hadi minane, hii itasimamisha mazungumzo ya mateka.

Netanyahu ameapa kuwaangamiza Hamas na kuwarudisha mateka wote nyumbani, lakini malengo hayo bado hajayakamilisha hadi sasa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya