ZINAZOVUMA:

THAILAND kuwafata mateka wa HAMAS

Thailand yaanza mazungumzo ya kuwarudisha rai wake waliotekwa na HAMAS...

Share na:

Serikali ya Thailand kupitia waziri wa mambo ya Nje Parnpree Bahiddha-Nukara, wanatarajia kutembelea Misri na Qatar kwa mazungumzo.

Waziri huyo wa mamo ya nje anatarajiwa kuzungumza na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje nchini Qatar siku ya Jumanne.

Na anatarajiwa kuzungumza na waziri wa mambo ya nje wa Misri siku ya jumatano.

Lengo kuu la mazungumzo ya waziri huyo na mataifa hayo ni namna ya kuwaooa mateka 22 raia wa Thailand.

Mapigano hayo yamesababisha maafa makubwa kwa Israel, huku upande wa Gaza ukiteketea zaidi.

Pamoja na vifo vya wati zaidi 9000, watoto wakifikia takrian theluthi ya vifo hivyo, na majeruhi wasiohesabika katika ukanda huo kwa Gaza na Israel.

Huku Hamas wakiteka raia wa mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Israel, Thailand, Argentina, Brazil, Marekani, Ufaransa, Russia pamoja na Nepal.

Huku wengi katika mateka hao wakiaminika kuwa na uraia pacha wa Israel na nchi nyingine, ingawa inasemekana kuwa baadhi ya raia wa Thailand na Nepal hawana uraia pacha.

Waziri mkuu wa Thailand Srettha Thavisin, amesema kuwa serikali yake inafanya juhudi kubwa kuwarudisha nyumbani raia wake.

Serikali yake pia nawalipa raia wake ambao wameathirika na vita hivyo, bila kujali bado wapo Israel au wamerudi Thaland.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya