Serikali ya Tanzania kujenga nyumba 101 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na maporomoko ya tope zito kutoka mlima Hanang. Mafuriko ambayo yamepelekea vifo vya watu 89 na zaidi ya watu 100 kujeruhiwa. Katika kuongeza nguvu katika juhudi hizo za Serkali Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania linaendelea na ujenzi wa nyumba 35 kwa waathirika hao ikiwa ni moja ya hatua ya kuisaidia jamii.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Shirika hilo David Kihenzile, wakati akisoma barua ya pongezi kutoka kwa Rais Samia kwenda kwa shirika hilo ya kuwapongeza kwa namna ambavyo walijitoa kuwasaidia wahanga wa maafa hayo mkoani Manyara na kusisitiza kuwa wamekuwa wakiishi kanuni saba za shirika hilo ikiwemo ubinadamu na kujitolea.
Maporomoko ya tope zito mkoani Manyara yalitokea asubuhi ya Desemba 3 mwaka jana.