ZINAZOVUMA:

Mafuriko Hanang, vifo vyaongezeka

Wilayani Hanang, vifo vingi vimetokea kutokana na mafuriko pamoja na...

Share na:

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko na matope katika mkoani Manyara imeongezeka kutoka 23 hadi 47.

Vifo hivyo mkoani humo, vimesababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua za siku ya Jumapili.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sengida, ameongeza kuwa Operesheni ya uokoaji zitaendelea usiku kucha, na idadi ya majeruhi ni 85 hadi jana jumapili jioni.

Pia aliyataja maeneo mengine yaliyoathirika na mafuriko pamoja na matope hayo kuwa ni pamoja na Mji wa Katesh na vijiji vya Jorodom, Gendabi, Mogito na Gedan’gonyi.

Na kuongeza kuwa Kuna kijiji kimezama kabisa kutokana na tope lililoshuka kutoka milimani.

Afisa wa Taasisi ya Jiolojia Tanzania Gabriel Mbogoni, amesema kuwa wametuma wataalamu kuchunguza tukio hilo.

Onyo la mvua kali za kipindi hiki cha vuli kwa miezi ya Septemba hadi Disemba, lilikwisha tolewa na mamlaka ya hali ya Hewa nchini.

Huku taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa ikisema kuwa kuna uwezekano wa El Nino kipindi hiki na madhara yake ni makubwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya