ZINAZOVUMA:

‘Tiktok’ na ‘Telegram’ zapigwa marufuku Somalia

Wizara ya Mawasiliano nchini Somalia imeagiza mamlaka inayosimamia intaneti kuzima...

Share na:

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia nchini Somalia imeagiza mamlaka inayoratibu utoaji wa huduma za intaneti nchini humo kuzima uwezo wa kufikia mitandao ya kijamii ya TikTok, Telegram, na tovuti ya kamari ya 1xBet.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Jama Hassan Khalif alitoa agizo hilo katika taarifa yake huku akitaja sababu za kuzuia makampuni hayo kuwa ni usalama na kupambana na ugaidi.

Taarifa hiyo ilisema ukiukwaji wa mara kwa mara wa sheria kwa makundi ya kigaidi yanayotumia mitandao ya kijamii ikiwemo ya Tiktok na Telegram huathiri usalama na utulivu wa jamii.

Wizara hiyo imesema inafanya kazi kulinda maadili ya watu wa Somalia wakati wa kutumia njia za mawasiliano ya mtandaoni ambazo zimeathiri mfumo wa maisha na kuongeza kile ilichosema ni tabia mbaya, kulingana na taarifa hiyo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,