Umoja wa wafanyabiashara na wamiliki viwanda na Kilimo TCCIA kwa kishirikiana na muwekezaji kutoka visiwa vya Comoro wamezindua meli ya abiria ambayo inatarajiwa kufanya kazi katika bandari ya Mtwara.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Raisi wa Umoja wa TCCIA Swallah Said Swallah ambapo amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 300 na mizigo mchanganyiko wa vyakula tani 150.
Amesema meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake mara mbili kwa mwezi ikileta abiria pamoja na mazao ya biashara kutoka Comoro hadi Mtwara na kutoka Mtwara kwenda Comoro.
Aidha amewataka wafanyabiashara wa Mtwara kuchangamkia fursa ya kupeleka bidhaa za biashara hususani vyakula na mazao yote yanayolimwa kwenye mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara.