ZINAZOVUMA:

Mtwara Baada ya Ziara ya Mama

Mama apnagua safu ya mkoa wa Mtwara, kuanzia RAS, ...
Katibu Tawala mteule wa Mkoa wa Mtwara

Share na:

Siku chache baada ya ziara ya mama Mikoa ya Lindi na Mtwara, ametengua na kuteua wafuatao katika nafasi mbalimbali mkoani Mtwara.

Ametengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Tawala Bw. Abdallah Mohamed Malela, Na Kumteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kushika nafasi hiyo mkoani humo. Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya Mtwara Mjini, Bw. Hanafi Msabaha, na kumteua Bi. Mwanahamisi Mkunda katika nafasi hiyo. Bi Mkunda alikuwa mkuu wa wilaya ya Temeke kabla ya uteuzi wa leo.

Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kushika nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Huku Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mariam Chaurembo akingoja kupangiwa kazi nyingine.

Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC, huku Kanali Emmanuel Mwaigobeko akingoja kupangiwa kazi nyingine. Bw. Nyange alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo.

Amemteua bw. Abeid Abeid Kafunda kushika nafasi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara (Mtwara DC), baada ya kutengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike aliyekuwa akishika nafasi hiyo. Bw. Kafunda ameteuliwa katika nafasi hiyo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali alipokuwa akihudumu kama mwanasheria.

Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, huku aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella akingoja kupangiw akazi nyingine.

Na mwisho memteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ya Namtumbo. Ndugu alikuwa Katibu Tarafa wa Mswaki wilaya ya Handeni kabla ya uteuzi huu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya