ZINAZOVUMA:

Spika Tulia Ackson aukwaa uraisi wa maspika wa dunia

Spika wa Bunge la Tanzania Bi Tulia Ackson awabwaga wenzake...

Share na:

Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, amechaguliwa kuwa raisi wa umoja wa mabunge duniani (IPU).

Spika Tulia amechaguliwa kushika wadhifa huo, leo tarehe 27 Oktoba 2023 katika kongamano la umoja huo Jijini Luanda nchini Angola.

Amepata nafasi ya kuwa raisi wa 31 katika umoja huo kwa kushinda kura 172 kati ya 303 zilizopigwa.
Wengine waliokuwa wakipambania nafasi hiyo ni Bi Adji Mergane Kanoute wa Senegal aliyepata kura 52, Bi Catherine Gotani Hara wa Malawi aliyepata kura 61 na Bibi Marwa Abdibashir Hagi kutoka Somalia aliyepata kura 11.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,