ZINAZOVUMA:

Spika azuia mjadala mkataba wa ‘dp world’

Spika wa Bunge Dkt Tulia Akson ametoa muongozo kuhusu mjadala...

Share na:

Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson amezuia mjadala wa sakata la bandari kuzungumzwa bungeni lakini akaruhusu kuwa litakapokuja kwa utaratibu mwingine wa kibunge itakuwa ruksa.

Spika Dkt Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 29,2023 muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya wabunge ambapo amesema kuwa Bunge lilishamaliza mjadala huo hivyo wabunge wanatakiwa kuendelea kuwasikiliza wananchi.

Aidha ameweka wazi kuwa kazi iliyobaki ni kuisimamia serikali katika kufanya maamuzi ambayo tayari Bunge lilikua limeshapitisha hapo awali.

Pia ameongeza Kwa sasa wabunge wabaki wawasikilize wananchi na kama itatokea serikali itapeleka tena mkataba ujadiliwe Bungeni ndio wabunge wanaweza kujadili kupitia maoni wanayoyasikia kutoka kwa wananchi.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya