ZINAZOVUMA:

Shekhe Ponda na wengine 9 wakamatwa

Shekhe Ponda akamatwa na Kikosi cha Kanda Maalum Mkoa wa...

Share na:

Shekhe Ponda Issa Ponda Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu akamatwa katika maandalizi ya maandamano yenye jina “Matembezi ya amani”, kupinga mauaji yanayoendelea dhidi ya wapalestina yaliyotarajiwa kufanyika leo tarehe 10 Novemba 2023.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata watu 10 akiwemo na Sheikh Ponda maeneo ya Mnazi mmoja.

Maandamano hayo yaliyokuwa yakisimamiwa na Shekhe Ponda, yalilenga kupaza sauti na kupinga mauaji yanayofanywa na wazayuni dhidi ya wapalestina.

Maandamano hayo yaliyotarajiwa kuanza Mnazi Mmoja na watu hao kutembea hadi Manzese Tip Top.

Hata hivyo punde baada ya watu hao kufika maeneo hayo ya Mnazi Mmoja, walikamatwa na Polisi wakiwemo waliovalia kiraia.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema polisi inawashikilia wanawake wanne na wanaume sita.

Na kuongeza kuwa hawajajua lengo kuu la mkusanyiko huo, ila watawahoji na wataendelea na taratibu zinazofuata baada ya mahojiano.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,