ZINAZOVUMA:

Shaka: Amemuua mkewe na kumfukia chumbani

Polisi wanamshikilia mwanaume aliyemuua mkewe na kumfukia chumbani mwao. Hayo...

Share na:

Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Mohamed Omar (37) mkazi wa kijiji cha Kimamba “A” wilayani kilosa kwa tuhuma za kumuua mkewe aliyetambuliwa kwa jina la Beatrice Haiyasi na kumzika ndani ya chumba chao cha kulala.

Mkuu wa wilaya ya Kilosa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Shaka Hamdu Shaka amesema tukio hilo la mauaji lilifanyika Januari 1, mwaka huu (2024) baada ya mtuhumiwa huyo kumpiga na kisha kumzika mkewe ndani ya chumba chao.

“Baada ya kumuua alichimba shimo lenye urefu wa futi mbili na nusu katika chumba ambacho walikuwa wakilala na kumfukia. Baada ya kumfukia aliendelea kuishi kwenye chumba hicho na eneo ambalo ameufikia mwili huo.” na kuongeza kuwa mtuhumiwa aliamua kuweka mafiga katika eneo hilo ili majivu yaendelee kupoteza ushahidi.

Shaka alisema kuwa chakusikitisha kabisa, alianzisha mahusiano na mwanamke mwingine.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,