ZINAZOVUMA:

Serikali yawasilisha pingamizi kesi ya bandari

Serikali ya Tanzania imewasilisha pingamizi lake la kuitaka Mahakama Kuu...

Share na:

Serikali imewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, yanayohusisha uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiiomba Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya isisikilize.

Kesi ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 imefunguliwa na wanasheria wanne Alphonce Lusako, Emmanuel Kalikenya Changula, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi, wakipinga makubaliano hayo, wakidai kuwa baadhi ya ibara zina masharti mabovu ambayo hayana maslahi kwa taifa.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo Alhamis Julai 20, 2023 na jopo la majaji watatu linoloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.

Hata hivyo Serikali katika majibu yake ya maandishi iliyoawasilisha mahakamani hapo imeibua pingamizi la awali ikiiomba mahakama hiyo iitupilie mbali kesi hiyo kabla ya kuisikiliza.

Kutokana na kuwepo kwa pingamizi hilo la awali, kiutaratibu mahakama inapaswa kuanza kulisikiliza kwanza pingamizi hilo na kulitolea uamuzi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya