ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu amesema Bandari haitauzwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema wananchi wanatakiwa kuwa na imani...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameomba Watanzania waiamini Serikali kwenye uwekezaji unaotaka kufanyika katika Bandari, akidai kuwa uwekezaji huo sio wa kwanza wala sio jambo jipya.

Waziri Mkuu amesema kuwa kulikuwa na mabakubaliano na mwekezaji ambaye walimpa vipindi vya kumfanyia tathmini hadi akafika miaka 22 na ameondoka Novemba mwaka 2022,hivyo DP World nao watampa vipindi kama aliyekuwepo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Mwekezaji huyu mpya hajauziwa bandari, ila atapewa kuwekeza.

Kuhusu ukomo wa muda, amesema wanaodai DP World kapewa miaka 100 au milele sio kweli kwani hapajaandikwa popote juu ya ukomo ila akija ndio watakubaliana juu ya suala hilo.

Ameongeza kuwa Mwekezaji hajauziwa ardhi kwani hata sheria za nchi haziruhusu ila mwekezaji atapewa kibali cha kukaa juu ya ardhi na atalipa kodi, pia mkataba utazingatia maslahi ya nchi kama wengi wanavyodai.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya