ZINAZOVUMA:

Rangi za nywele zasababisha apigwe faini Urusi

Kijana mkaazi wa Moscow awekwa rumande na kupigwa faini kwa...

Share na:

Moja ya habari iliyo washangaza wengi ni ya kijana mmoja mjini Moscow, Kupigwa faini na kufunguliwa mashtaka na polisi kwa kupaka nywele zake rangi ya njano na bluu ambazo ni za bendera ya Ukraine.

Usiku wa Aprili 27, Stanislav Netesov alishambuliwa na watu wasiojulikana, kwenye kituo cha basi katikati ya mji wa Moscow alipokuwa akirejea kutoka kazini.

Aliibiwa simu na kung’olewa jino katika shambulio la usiku huo, na alishangazwa alipokwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika wilaya ya Tverskoy baada ya kuwekwa rumande.

Na sababu iliyomfanya awekwe rumande ni kuweka rangi za bendera ya Ukraine katika nywele zake.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,