ZINAZOVUMA:

RAISI WA ANGOLA ATEUA GAVANA MPYA

Rais wa Angola, Joao Lourenco, amteua Manuel Tiago Dias kuwa...

Share na:

Rais wa Angola, Joao Lourenco, amemteua Manuel Tiago Dias kushika wadhifa wa gavana wa benki kuu, kulingana na taarifa ya serikali iliyotolewa siku ya Ijumaa.

Dias alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Angola kabla ya uteuzi wake na atachukua nafasi ya Jose de Lima Massano, ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa uratibu wa uchumi wa nchi hiyo wiki iliyopita.

Massano aliteuliwa kuwa waziri wa uratibu wa uchumi baada ya maandamano yenye ghasia yaliyotokea kutokana na kupunguzwa kwa ruzuku ya mafuta hali iliyopelekea kuongezeka kwa gharama za mafuta na nishati nchini humo.

Tangu ashinde mhula wake wa pili wa urais mwezi Agosti mwaka jana, Lourenco ameahidi kuendeleza mageuzi ikiwa ni pamoja na kubinafsisha mashirika ya serikali yanayofanya vibaya pamoja na kupambana na ufisadi.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya