ZINAZOVUMA:

Raisi Mwinyi atengua wawili visiwani

Raisi Mwinyi atengua teuzi mbili, ya Kamisha wa Wizara ya...
Raisi Mwinyi akisisitiza jambo

Share na:

Raisi Hussein Ali Mwinyi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, atengua watu wawili katika nyadhifa zao visiwani humo.

Kutokana na taarifa kutoka Ikulu, Raisi Mwinyi ametengua uteuzi wa Bi. Saumu Khatibu Haji na Mhandisi Makame Ali Makame.

Bi. Saumu alikuwa alikuwa kamishana wa Bajeti, Ofisi ya Raisi, Fedha na Mipango.

Bi. Saumu amehudumu kama kamishna wa Bajeti kwa muda wa takriban miaka miwili, tangu alipoteuliwa mwezi Septemba 2021.

Na Mhandisi Makame alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROAD).

Mhandishi Makame amehudumu katika cheo hicho kwa miezi miwili, tangu alipoteuliwa kwenye wadhifa huo Tarehe 27 mwezi Juni 2023.

Hata hivyo taarifa hiyo ya kutoka Ikulu, haijasema sababu za utenguzi wa viongozi hao wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya