ZINAZOVUMA:

Oryx wamwaga mitungi kagera

Oryx Gas Tanzania wagawa mitungi ya gesi kwa mama ntilie,...
Oryx wakigawa mitungi mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi. fatma Mwasa akigawa mitungi ya Oryx kwa wafanyakazi wa Afya, mama ntilie na walimu Mkoani humo.

Share na:

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bi. Fatma Mwasa, aliungana na Bi. Antonia Kilama Kutoka Oryx Gas Tanzania LTD, katika ugawaji wa mitungi ya gesi uliofanyika katika Mkoa wa Kagera.

Wanufaika wa jitihada hiyo ya Oryx ni walimu, wafanyakazi wa afya, na mama ntilie wa mkoani humo.

Mitungi hiyo ilitolewa kwa watu wachache kutoka katika makundi tajwa hapo juu, kama wawakilishi wa makundi lengwa kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Kagera.

Bi. Maswa alishukuru kwa kampuni hiyo ya Oryx kwa kuweka mkoa wa Kagera katika maeneo yatakayoguswa na kampeni hiyo ya kugawa mitungi.

Lengo la Kampeni hiyo ni kuunga mkono ajenda ya serikali, ya kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa upande mmoja, na kuongeza matumizi ya nishati safi kwa upande wa pili.

Katika kusisitiza ajenda ya serikali ya awamu ya sita, Mkuu wa mkoa alihimiza wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa kama nishati za kupikia.

Mbali na msisitizo huo alieleza kwamba kuepuka nishati hizo itasaidia kuimarisha afya ya wanajamii, na itasaidia uhifadhi wa mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Bi. Antonia Kilama alisema, “Oryx ina nia ya dhati ya kusaidia Watanzania, haswa wanawake ambao wanathiriwa zaidi na matumizi ya kuni na makaa ya mawe.”

Kwa ufafanuzi zaidi, Bi. Kilama alisema nia kuu ya Oryx ni kusaidia harakati za kuongeza matumizi ya nishati safi kufikia 80% ifikapo mwaka 2030 kama ilivyoelezwa na Rais Samia.

Bi. Kilama alimuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oryx gas Tanzania LTD katika hafla hiyo mkoani Kagera.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya