ZINAZOVUMA:

Rais Samia kuongoza kumbukizi ya 40 ya Sokoine

Rais Samia anatarajia kuongoza kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati...

Share na:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa anatarajia kuongoza watanzania katika kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.

Akizungumza na wanahabari mjini Arusha, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaomba wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika maadhimisho hayo.

Mkuu wa mkoa amemtaja Hayati Sokoine kama mtu aliyekuwa muadilifu na mchapakazi, huku akiwataka watanzania kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwaenzi viongozi waadilifu na wachapakazi wa sasa wenye sifa za uchapakazi wa kufanana na Waziri Mkuu huyo.

Makonda amemtaja Hayati Sokoine kama mtumishi mahiri na mwenye ujasiri wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya watanzania bila kuogopa na kuhofia vikwazo mbalimbali.

Mkuu wa mkoa ametembelea makazi ya hayati Sokoine eneo la Enguiki Monduli, kukagua maandalizi ya kumbukizi ya miaka 40 tangu kifo chake.

Hayati Moringe alikuwa Waziri Mkuu mara mbili, mara ya kwanzani kuanzia tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, an alikuja kushika nafasi hiyo tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake,

Hayati Edward moringe Sokoine alifariki kwa ajali ya gari katika barabara ya Dodoma Morogoro ndani ya mkoa wa Morogoro.

Uongozi wake unatajwa kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya