ZINAZOVUMA:

Rais Samia ahimiza upendo na ustahimilivu

Rais Samia ahimiza upendo, Umoja, mshikamano paoja na kuliombe ataifa...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Sikukuu ya Pasaka, huku akisisitiza upendo, umoja na mshikamano katika jamii.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Rais Samia ameandika: “Kheri ya Sikukuu ya Pasaka kwenu nyote. Katika siku hii ambayo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, tuendelee kujifunza katika upendo wake mkuu wa kujitoa kwa ajili ya wengine”.

Aliendelea kusema tuwe na upendo kwa muumba wetu, kwa ndugu, jamaa na jirani zetu, na utusukume kuishi katika njia iliyo njema na kuendelea kuliombea Taifa letu amani, umoja na mshikamano.

“Upendo kwa wale tunaotofautiana nao, utusukume kutafuta na kuishi katika maridhiano na ustahimilivu. Upendo kwa nchi yetu, utusukume kuitumikia kwa weledi na kila wakati kukusudia kupiga hatua mbele zaidi kwa kujenga upya.”

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya