ZINAZOVUMA:

PAPA FRANCIS: Amani hailetwi na silaha

Papa akemea vikali Mashambulizi ya Ukanda wa Gaza pamoja na...

Share na:

Papa Francis ametoa wito mkali wa kusitishwa kwa vita huko Gaza na Ukraine.

“Amani haifanyiki kwa silaha,” Papa alisema katika ujumbe wake wa Pasaka mjini Vatican.

Alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza – pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.

Papa alikuwa akiongoza sherehe ya pasaka huko Vatican. Sherehe hizo zimekuwa zikifanyika kote ulimwenguni kuadhimisha sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya Kikristo.

Makumi ya maelfu ya waumini wamekusanyika katika uwanja wa St Peter’s Square kumsikiliza Papa Francis akiongoza Misa ya Jumapili ya Pasaka.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya