ZINAZOVUMA:

Putin ahofia kwenda Afrika Kusini

Raisi wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa Raisi wa...

Share na:

Raisi wa Afrika Kusini amesema kuwa Raisi wa Urusi, Vladimir Putin hatohudhuria mkutano wa nchi za BRICS utakaofanyika Afrika Kusini mwezi ujao.

Taarifa hiyo imekuja mara baada ya Raisi Cyril Ramaphosa kusema kuwa kumkamata Raisi Putin itakua ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Urusi.

Raisi Ramaphosa alisema hivyo sababu kama Putin angeondoka nchini kwake basi angetakiwa kukamatwa na kwa mujibu wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC Afrika Kusini ingetakiwa kusaidia katika mchakato huo sababu imetia saini ya makubaliano na Mahakama hiyo.

Kwa niaba ya Raisi wa Urusi, waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov, atamuwakilisha katika mkutano huo wa siku mbili.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa Raisi Putin atajumuika na viongozi wenzake katika mkutano huo unaounganishwa na nchi za Brazil, Urusi, India, China, pamoja na Afrika Kusini.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya