Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema anataka kuona amani ikitawala lakini nchi za Magharibi zinapandikiza mbegu ya chuki dhidi ya nchi hiyo.
Akihutubia katika siku ya mashujaa amewapongeza wanajeshi wanaoshiriki kwenye alichokiita operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kuwa hatma ya dola ya Urusi inawategemea wao.
Aidha Putin mara kwa mara amekuwa akiifananisha Ukraine ni kama serikali iliyochaguliwa kidemokrasia na wanazi walioshindwa katika vita vya Pili vya Dunia.
Hajaachana na kauli hiyo leo pia huku akiendelea kuwashutumu viongozi wa Ukraine kama wanazi mamboleo na kusema kuhusu “vita vya kweli” vinavyoendeshwa dhidi ya nchi ya Urusi.