ZINAZOVUMA:

Zelenskiy ataka dunia iungane dhidi ya Urusi

Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameitaka dunia kuungana ili kumzuia...

Share na:

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema kuwa changamoto nyingne za kidunia ni rahisi kutatuliwa baada ya Urusi kuzuiwa uvamizi wake ndani ya Ukraine.

Zelensky ameyasema hayo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, huku akihimiza ulimwengu kuungana ili kukomesha uchokozi wa Urusi dhidi ya nchi yake.

Katika hotuba yake yenye hisia kali mjini New York Zelensky alisema Urusi ina miliki silaha za nyuklia na ni lazima ikomeshwe ili isisababishe ulimwengu kuingia vitani.

Katika hotuba ambayo iliangazia sana madhara yanayoletwa na Urusi kwa ulimwengu, Zelenskiy alisema kuwa changamoto zingine za kawaida kama vile mabadiliko ya hali ya hewa zinaweza kushughulikiwa ipasavyo baada ya Urusi kurudishwa nyuma.

“Wakati Urusi inasukuma ulimwengu kuingia kwenye vita vya mwisho vya dunia, Ukraine inafanya kila kitu kuhakikisha kuwa baada ya uchokozi wa Urusi hakuna mtu ulimwenguni atakayethubutu kushambulia taifa lolote,” Zelensky alisema

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya