ZINAZOVUMA:

Nyara za Serikali zawasababishia kifungo cha miaka 20

Mahakama imewapa adhabu ya miaka 20 jela kwa kila mmoja...

Share na:

Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kukutw ana hatia ya kuwa na nyara za Serikali wakazi wawili wa wilaya hiyo.

Watu hao waliohukumiwa kifungo hicho ni Paulo John (23) Mkazi wa kijiji cha Mapea, kata ya Magugu na Athumani Misanya (31) Mkazi wa kata ya Mamire baada kukutwa na nyara za serikali ikiwemo kichwa cha Twiga.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu wa Mahakama hiyo, Victor Kimario baada ya kusikiliza hoja za pande zote.

Katika hukumu hiyo amesema kuwa “amejiridhisha pasina shaka juu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri, hivyo kwa kuzingatia kuwa wakosaji ni wa mara ya kwanza licha ya kuwa vijana wadogo, lakini wametumia nguvu zao vibaya kuihujumu Serikali, hivyo amewahukumu kwenda Jela miaka 20 kila mmoja huku vifaa vilivyotumika kubebea nyara hizo (Ndoo na Pikipiki) kutaifishwa, pamoja na kuwapa haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia leo”.

Awali waendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Getrude Kariongi na Shaidu Kajwangya wakishirikiana na wakili Mwanaidi Chuma wamesema washtakiwa hao wanadaiwa kutenda Kosa hilo 02/02/2024 katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge

Wamesema washtakiwa hao walikutwa na Kichwa, Mkia, ngozi vyote vya twiga pamoja na nyama ambayo inaaminika itakuwa ya twiga, vikiwa kwenye ndoo wakiwa na usafiri wa pikipiki.

Ambapo thamani ya Twiga huyo ikiwa ni zaidi ya shilingi Milioni 50, wameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu ili kufikisha ujumbe kwa jamii na watu wenye kufanya makosa ya ujangili, ili kukomesha vitendo hivyo kwani Mnyama Twiga ni nembo ya Taifa lakini pia ni kivutio cha Utalii unaoingizia nchi mapato.

Kwa upande wake Wakili wa utetezi Festo Jackson ameiomba mahakama Kwa kuwa watuhumiwa hao ni wakosaji wa mara ya kwanza na Umri wao bado ni mdogo na wapo na wategemezi wanao wategemea hivyo Mahakama iwaonee huruma na kuwapunguzia adhabu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya