ZINAZOVUMA:

Bodi ya Utalii yatangaza fursa kanda ya kusini

Regrow wawezesha Bodi ya Utalii kuwakutanisha wadau wa Utalii kutoka...

Share na:

Bodi ya utalii nchini (TTB) imewakutanisha mawakala wa safari za watalii kutoka Ujerumani na Wadau utalii kanda ya kusini mwa Tanzania, ili kuongeza matangazo ya vivutio vya utalii vinavyopatikana ukanda huo na kuongeza idadi ya wageni wa kuvitembelea.

Katika mahojiano Afisa Habari wa bodi hiyo kanda ya kusini, Hoza Mbura amesema lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kuwafanya mawakala wa nje kufahamu vivutio vya Utalii kanda ya Kusini ili walete wageni na kuongeza ushirikiano na wadau wa biashara hiyo kutoka Kusini.

Bi. Beatrice Massawe mmoja wa washiriki wa Mkutano huo ulioandaliwa na TTB kwa ufadhili wa REGROW ameishukuru bodi hiyo kwa kuwakutanisha na mawakala hao wa utalii kutoka Ujerumani.

“kiukweli tumeanza kupata mwanga mwingine na tunawakaribisha pia Watanzania watembelee vivutio hivi vya utalii kusini kwa sababu hawa mawakala wametoka Ujerumani kwa ajili ya kuja kutusaidia sisi kututangasia nchi yetu hasa ukanda wa kusini“ Amesema Beatrice Masawe

Vilevile baadhi ya mawakala hao kutoka Ujerumani wamesema “lengo la kutangaza Utalii wa kusini mwa Tanzania ukiwa ujerumani ukanda huu wa kusini unafahamika sana na maeneo mengi watalii wameshatembelea kama hifadhi ya Taifa Ruaha na tumefurahishwa na uzuri wa eneo hilo hasa ukijani wa Asili“

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya