ZINAZOVUMA:

Niger: aondoke ndani ya saa 72

Baada ya Serikali ya kijeshi nchini Niger kuzuiwa kuhudhuria Mkutano...

Share na:

Baada ya serikali ya kijeshi ya Niger kuzuiwa kuhutubia katika mkutano wa 78 wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), wametoa saa 72 za Louise Aubin kuondoka nchini humo.

Waziri wa mambo ya Nje wa Niger amesema kuwa Umoja wa Mataifa umetumia vikwazo vingi kuwazuia kuhudhuria mkutano huo.

Huku bwana Stéphane Dujarric, akisema kuwa Katibu Mkuu hana maamuzi juu ya nani ahudhurie na nani asihudhurie, maamuzi hayo hutoka kamati inayochambua sifa za washiriki wa mkutano huo.

Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN amesema kuwa Hata Burma (Myanmar) na Afghanistan zimekuwa zikiwakilishwa na wajumbe wa zamani.

Nchi hizo kuwakilishwa na wajumbe wa zamani ni kutokana na kamati hiyo ya kuchuja sifa za washiriki haijapitisha nchi hizo kama washiriki wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya