Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kupanda jukwaani katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza na kuhutubia mbele ya viongozi wa nchi mbalimbali, juu uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake.
Mwaka mmoja uliopita, Zelenskiy aliidhinishwa kwa hali ya kipekee kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Zelenskiy atashiriki mkutano huo wa ngazi ya juu wa kila mwaka siku ya leo Jumanne na mkutano maalum wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, kabla ya kuondoka kuelekea Washington ambako atapokelewa katika Ikulu ya Marekani siku Alhamisi.
“Kwetu sisi ni muhimu sana maneno yetu, ujumbe wetu wote usikike na washirika wetu,” alisema Zelenskiy siku ya Jana Jumatatu wakati akizungumza na wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa.