Mchezaji wa klabu ya Yanga Clement Mzize amesilimu na kuingia katika uislamu hii leo nyumbani kwa Kaimu Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omary.
Mzize amefikia hatua hiyo ikiwa ni siku ya kwanza ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuanzia sasa atafahamika kwa jina la Walid Mzize.
Video mbalimbali zimemuonyesha mchezaji huyo akiwa nyumbani kwa Sheikh Walid akifundishwa baadhi ya mafunzo na miongozo katika uislamu.
Mashabiki na waumini wa dini ya kiislamu wamempongeza mchezaji huyo kwa hatua hiyo aliyoifanya ya kubadili dini kutoka ukristo kwenda Uislamu.