ZINAZOVUMA:

Simba na Yanga wapangiwa vigongo michuano CAF

Baada ya droo kufanyika hii leo hivi ndio vigongo walivyopangiwa...

Share na:

Droo ya mechi za Awali za Klabu Bingwa Barani Afrika CAF ,imepangwa leo Julai 25, 2023 na tayari ratiba imetolewa kwa timu zinazoshiriki klabu Bingwa.

Ratiba ya klabu Bingwa kwa timu zinazotoka Tanzania ipo hivi, KMKM ya Zanzibar itacheza dhidi ya St George ya Ethiopia na mshindi atacheza dhidi ya Bingwa Mtetezi Al Ahly ya Misri.

Wakati timu ya Yanga itacheza dhidi ya timu ya ASAS kutoka Djibouti na mshindi wa mechi hiyo atakutana na mshindi katika mechi ya El Merrikh ya Sudan dhidi ya Otoho ya Congo.

Na Kwa upande wa Simba ambae ataanzia round/awamu ya pili itakutana na mshindi katika mechi ya Af. Stars ya Namibia dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Mechi hizo zitachezwa kati ya Agosti 18, 19, na 20 kwa mechi ya kwanza na mechi za marudiano ni kati ya Agosti 25, 26 na 27.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya