ZINAZOVUMA:

Mwili wa mwanafunzi waokotwa vichakani

Mwili mwanafunzi wa darasa la sita umekutwa vichakani baada ya...

Share na:

Mwanafunzi wa darasa la sita Kilima Elius Antony, katika shule ya Msingi Kilima iliyopo kitongoji cha Mwizi Kata ya nyakato, wilaya ya Bukoba Vijijini, ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mwili wake kutelekezwa kichakani.

Tukio hilo limethibitishwa kutokea na Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera Brasius Chatanda.

Kamanda Chatanda amesema amepokea taarifa ya tukio hilo leo tarehe 13 April, 2024 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilima, Izidory Kaiza amesema alipokea taarifa za kupotea kwa mwanafunzi huyo, kwenye kitongoji cha Mwizi tangu April 10 kutoka kwa wazazi wake, ndipo walipoanza kumtafuta hadi mwili wake ulipopatikana.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya