ZINAZOVUMA:

Shule yaungua Bukoba

Zimamoto mkoani Kagera wamefanikiwa kuzuia Moto usiteketeze shule ya sekondari...

Share na:

Askari wa kikosi cha Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kagera wamefanikiwa kudhibiti moto usiendelee kuteketeza majengo mengine katika shule ya sekondari ya Istiqama Manispaa ya Bukoba.

Moto huo umetokea jana Ijumaa Julai 7, 2023 saa 12 kamili jioni. Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji mkoani hapa, Zabron Muhumha amesema baada ya jeshi hilo kupata taarifa askari wa jeshi hilo waliwahi eneo la tukio kwa ajili ya kuudhibiti.

“Baada ya kupata taarifa ya moto huo askari wangu wamewahi eneo la tukio wakiwa na gari letu na baadae wameongeza nguvu kwa kutumia gari la uwanja wa ndege na kufanikiwa kuudhibiti moto huo ili usiendelee kusambaa na kuleta madhara zaidi” amesema Muhumha

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Farid Said amesema, bweni lililoungua lilikuwa la wavulana, huku mpaka Sasa hakuna madhara yoyote kwa binadamu (majeruhi) yaliyosababishwa na moto huo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya