ZINAZOVUMA:

Mufti kuelekea Saudia leo

Mufti Zuberi wa Tanzania anatarajia kusafiri kuelekea nchini Saudi Arabia...

Share na:

Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili tarehe 21 Aprili 2024 kuelekea jijini Riyadh nchini Saudi Arabia.

Taarifa imetolewa na mkurugenzi wa Mambo ya nje wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) sheikh Twahir Almusawwa.

Taarifa hiyo imesema kuwa Katibu mkuu wa Taasisi ya Muslim World League Dkt. Muhammad Abdul Kareem Al-iisa amemualika Mufti Zubeir, baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa kudumu wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ya waislamu Ulimwenguni.

Kwenye Safari hiyo Mufti ataambatana na Sheikh Musaawa pamoja na Sheikh Othman Kaporo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,