ZINAZOVUMA:

Waislamu wahamaki sheria LGBTQ Kenya

Viongozi wa dini ya kiislamu nchini Kenya wamepinga maamuzi ya...

Share na:

Viongozi wa dini ya Kiislamu Mombasa nchini Kenya wamekemea na kupinga uamuzi wa Mahakama juu ya uhuru wa haki ya wapenzi wa jinsia moja na kuwaruhusu kujiandikisha kama shirika lisilo la kiserikali.

Viongozi hao wamesema kuwa uamuzi huo unakiuka maadili ya jamii za Kiafrika na mafunzo ya dini.

Wakizungumza na vyombo vya habari Mombasa, viongozi hao wameelezea hofu kwamba uhuru wa jamii hiyo, huenda ukachangia vijana wengi kujihusisha na masuala hayo ambayo yanakiuka dini, maadili na tamaduni za Kiafrika.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa baraza la maimamu Sheikh Muhammad Khalifa, amesema kwamba wao kama viongozi na Wakenya hawatambui uamuzi huo na kwamba ni sharti Rais na bunge la Kenya kuingilia kati kutumia sheria kupinga uamuzi huo.

“Tunamuambia Rais William Ruto yeye na naibu wake pamoja na wake zao, ni wakristo wanaokwenda kanisani, tafadhali hili ni jambo lakuharibu maadili ya nchi ya Kenya, na kuharibu heshima ya wananchi wa Kenya asilikubali na bunge pia lihakikishe hili jambo halitakuwa katika nchi ya Kenya,” Sheikh Muhammad Khalifa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya