ZINAZOVUMA:

Mabadiliko ya uongozi, uhamisho na uteuzi

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu...

Share na:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, uteuzi wa Mkuu wa Mkoa, uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na uteuzi wa Mkuu wa Wilaya kama siku ya leo tarehe 22/5/2023 kama ifuatavyo

Mhe Raisi Amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Mhe. Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya wakati Mzee Meja Jenerali atapangiwa majukumu mengine.

Raisi Samia amemuhamisha Mhe Queen Cuthbert Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya Mhe.Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.

Raisi Samia amemuhamisha Mhe.Charles Makongoro Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara.

Raisi Samia Amemteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo. Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.

Aidha Uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni, Ikulu Chamwino.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya