ZINAZOVUMA:

Msaada wa Kisheria kugaiwa bure Mkoani Njombe

Waziri wa Sheria Dkt. Pindi Chana na Mkuu wa Mkoa...

Share na:

Wizara ya Katiba na sheria imetoa wito kwa wananchi mkoani Njombe, kujitokeza katika maeneo mbalimbali yatakayopangwa kwa wanaohitajia msaada wa kisheria bila kulipia.

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito huo leo Mei 22, 2024, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Dkt. Chana ametoa tamko hilo katika uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa Kisheria, maarufu kama “Mama Samia Legal Aid Campaign” itakayo fanyika katika kituo cha mabasi cha zamani kuanzia Mei 26,2024.

“Na mgeni rasmi wa shughuli hii ya uzinduzi rasmi atakuwa ni Mhe Dotto Biteko Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, nitumie nafasi hii kuwaalika wananjombe wakaribie kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria.

Dkt. Chana aliongezea kuwa inafahamika kuwa wananchi wanachangamoto hivyo milango iko wazi.

Vile vile alisema kuwa “Kampeni hii itatekelezwa katika halmashauri zote za mkoa wa Njombe, yenye jumla ya kata sitini na vijiji mia na themanini kwa kipindi cha siku kumi”.

Huduma hizo zitatolewa na timu ya wataalamu kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali.

Katika kutangaza zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka, amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na Kampeni hiyo.

“Wananchi wote wenye malalamiko na wanahitaji msaada wa kisheria, tutumie wiki hii vizuri kwa kufika kwenye maeneo ambayo huduma hii inatolewa” amesema Mtaka.

Utekelezaji wa Kampeni hiyo ulianzia jijini atrehe 27 Aprili 2023 Dodoma ambapo ilizinduliwa tarehe 27 Aprili, 2023, na Zanzibar tarehe 9 Mei, 2023 ambapo Kwa sasa Kampeni hii imeufikia mkoa wa Njombe.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya