Kiwanda cha sukari cha Mkulazi mkoani Morogoro kimeanza uzalishaji disemba 23 mwaka.
Kiwanda hicho cha sita kujengwa nchini Tanzania, kinamilikiwa na Mfuko wa hifadhi ya jamii ya Taifa pamoja na Jeshi la Magereza.
Pia wanatarajia kuwa wa kwanza kuzalisha sukari ya viwandani (Industrial Sugar) nchini Tanzania chini ya nembo ya Mafao Sugar.
Kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha tani elfu hamsini (Tani 50,000) kwa mwaka.
Pia kiwanda hicho kimeorodheshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, kama sehemu ya uwekezaji wa kimkakati nchini.
Kabla ya Mkulazi kulikuwa na viwanda vitano vya sukari, kilombero Sugar, Mtibwa Sugar vinapatkana Morogoro, Kagera Sugar kinapatikana Mkoani Kagera, Bagamoyo Sugar kinapatikana Mkoani Pwani na TPC kinapatikana mkoani Kilimanjaro.
Viwanda vyote hivyo vinatarajiwa kupunguza utegemezi wa sukari kutoka Uganda, India Brazil na Thailand.