ZINAZOVUMA:

MKUDE awaburuza kina Mo mahakamani

Msukuma gozi kutoka klabu ya Yanga, Jonas Gerard Mkude awadai...

Share na:

Mchezaji wa timu ya Yanga Jonas Mkude “Mkude”, ameifikisha kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) mahakamani kudai fidia.

Mchezaji huyo amefikisha kampuni hiyo mahakamani, kwa kutumia picha yake kwenye matangazo bila ruhusa yake.

mcheza mpira huyo ameiomba mahakama kuiamuru, Metl kumlipa fidia ya Bilioni 1.

Ametetea fidia hiyo na kusema kuwa, amepata madhara ya kiuchumi na hata kisaikolojia, kutokana na kampuni hiyo kutumia picha zake.

Mbali na fidia, pia ambeomba mahakama iamuru apewe Mrabaha kutokana na faida waliyopata Metl kwa kutangaza kwa picha zake.

Kampuni ya uwakiliinayomuwakilisha Mkude katika kesi hiyo, ni Bridge Attorneys and Consultancy ya Jijini Dar es Salaam.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,