ZINAZOVUMA:

” Niliachwa na mwanamke wangu kisa Yanga”

Mchezaji wa Azam FC Feisal Salum amesema wakati wa sakata...

Share na:

Mchezaji wa klabu ya Azam FC Feisal Salum amefunguka wakati akifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari juu ya mambo aliyopitia wakati wa sakata lake dhidi ya waajiri wake wa zamani klabu ya Yanga.

Feisal amesema kuna vingi alivyopoteza kwa wakati ule lakini ameweka wazi kukimbiwa na mwanamke na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine wakati yeye akipitia kipindi kigumu.

“Lile sakata liliniathiri kwenye mambo mengi sana sio kwa upande wa kucheza pekee, wakati niko kwenye wakati mgumu kama ule kila wakati unafikiria hii kesi itaishaje, nikakutana na pigo lingine la kukimbiwa na mpenzi wangu ambaye niliamini ningekuja kumuoa.

“Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi.

“Ilikua ni hatua mbaya zaidi kwangu yeye kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata, sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu.” Alisema Zanzibar ‘finest’

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,