ZINAZOVUMA:

Matokeo ya Sensa wanyamapori na watalii hadharani

Wizara ya Utalii kupitia taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI)...

Share na:

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kutangaza rasmi Matokeo ya Sensa ya Wanyamapori, Pamoja na kuzindua ripoti ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea nchini kwa mwaka 2023.

Utangazaji na uzinduzi huu huo utajumuisha wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii utafanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha, ambapo Waziri wa maliasili na utalii Angellah Kairuki anayetarajiwa kutangaza matokeo hayo ya sensa na kuzindua ripoti hiyo.

Katika mkutano wake na wanahabari jijini Arusha, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Edward Kohi ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo na Mtafiti wa TAWIRI, amesema taarifa hizo zenye tija katika uhifadhi wa wanyamapori na kukuza utalii nchini zinaakisi juhudi za Serikali kuhifadhi utajiri wa Maliasili ya Wanyamapori na kukuza utalii nchini.

Aidha ripoti ya sensa hiyo ya itaangazia idadi ya watalii waliotembelea nchini mwaka 2023 baada ya filamu ya The Royal Tour.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya