ZINAZOVUMA:

Sanjay Duty apewa ubalozi wa utalii Tanzania

Muiigizaji kutoka nchini India Sanjay Dutt amepewa ubalozi wa kuitangaza...

Share na:

Serikali ya Tanzania imeeleza sababu ya kumchagua msanii wa filamu kutoka nchini India kuwa balozi wa heshima ni kutokana na mapenzi yake kwa nchi hii na kuwa na wafuasi wengi watakaoona na kusikia kuhusu fursa za utalii nchini.

Hayo yameelezwa jana Septemba 18 na Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Thereza Mugobi baada ya kumpokea msanii huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Amesema lengo la kumchagua Dutt ni kuingia kwenye soko la India yenye idadi ya zaidi ya watu bilioni 1.4.

“Msanii huyu ni mkubwa nchini India, ukifuatilia mitandao yake ya kijamii ana wafuasi zaidi ya 200 milioni. Hivyo tunaamini kwamba kituo cha Tanzania kitasikika katika soko la India na soko kubwa la Asia, ambako pia tunalenga kufikia huko,” amesema.

Maelezo hayo yameungwa mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale akisema kwa kumchagua msanii huyo watafanikiwa kupenya kwenye soko la utalii la India.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya